Baada ya kuitumikia Yanga kwa takribani misimu mitano, Farid Mussa amejiunga na klabu ya Coastal Union.
Wagosi wa Kaya jana walimtambulisha Farid kwenye Coastal Union Festival uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Farid ni miongoni mwa wachezaji walioanzisha urejeo wa mataji akijiunga na Yanga mwaka 2020 akitokea Hispania.
Amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichotwaa mataji matano mfululizo ya ligi kuu ya NBC, akiondoka na rekodi ya kushinda zaidi ya mataji 15 akiwa na Yanga.
Anaungana na mshambuliaji Emmanuel Mwanengo ambaye amerejea klabu ya TRA United
Kila la khri Farid...!
ADVERTISE HERE