Baada ya majadiliano ya wiki kadhaa inaelezwa klabu ya Al Ittihad imekubali ofa ya mwisho iliyotumwa na Yanga kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki.
Mapema leo Yanga ilimuuza mshambuliaji Laurindo Aurelio 'Depu' kwenda klabu ya Petro Atletico.
Mabilioni walioingiza kwenye mauzo ya Depu, yamewaongezea nguvu Wananchi kuweza kukamilisha usajili wa Aziz Ki.
Kwa muda mrefu Aziz Ki amesalia nchini akisubiri hatma yake, hatimaye klabu yake imetoa ruksa ajiunge na Yanga.
Mwamba huyo kutoka Burkina Faso sasa ni suala la muda atatambulishwa kujiunga na mabingwa hao wa nchi.
ADVERTISE HERE