Kipyenga cha ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2026/27 kinapulizwa rasmi leo, Ijumaa ya Agosti 14, 2026, huku macho ya wapenzi wa soka nchini yakielekezwa kwenye viwanja mbalimbali kushuhudia mzunguko wa kwanza.
Msimu huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali baada ya timu kufanya maboresho makubwa ya vikosi vyao.
Katika michezo ya leo, Pamba Jiji FC itawakaribisha Dodoma Jiji FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Mbeya City itapimana nguvu na Geita Gold FC kwenye Uwanja wa Sokoine, huku Singida Black Stars wakiwavaa Fountain Gate FC.
Ratiba ya Ijumaa, Agosti 14, 2026
- Pamba Jiji FC vs Dodoma Jiji FC β CCM Kirumba, Mwanza (Saa 8:00 Mchana)
- Mbeya City vs Geita Gold FC β Sokoine, Mbeya (Saa 10:15 Alasiri)
- Singida Black Stars vs Fountain Gate β Airtel Stadium, Singida (Saa 1:00 Usiku)

ADVERTISE HERE