katika tukio la kihistoria lililofanyika uwanja wa KMC Complex, Yanga imemtamulishwa rasmi kiungo mshambuliaj Stephane Aziz Ki mbele ya zaidi ya mashabiki 9000 walioujaza uwanja huo.
Aziz Ki anarejea Yanga akitokea klabu ya Al Ittihad ya Libya, Yanga ikitoa zaidi ya Bilioni 1.1 kumnunua kutoka klabu hiyo.
Ni usajili uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga kwani wanaufahamu uwezo wa mchezaji huyo ambaye kabla ya kuondoka Yanga aliweka rekodi ya kipekee ligi kuu ya NBC 2023/24 akitwaa tuzo ya MVP, mfungaji bora na mchezaji bora.
Aziz Ki anarejea Yanga kwa mara nyingine akichukua nafasi ya Allan Okello anayejiunga na klabu ya AS FAR ya Morocco.
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amethibitisha kuwa klabu imeridhia kumuuza Okello baada ya kupokea ofa nono.
Karibu tena Aziz Ki....!