Yanga vs Coastal Union: Kamwe awaita mashabiki kuijaza KMC Complex

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2026
Yanga vs Coastal Union: Kamwe awaita mashabiki kuijaza KMC Complex

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe, amewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa KMC Complex, kesho Alhamisi, Agosti 20, 2026, wakati Yanga itakapocheza mchezo wake wa kwanza wa nyumbani wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union.

Kamwe amesema licha ya Yanga kufanya usajili mkubwa katika dirisha lililopita, nguvu ya mashabiki bado ni sehemu muhimu katika kuipa hamasa timu hiyo na kuwahamasisha wachezaji kupambania nembo ya klabu.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe amesisitiza kuwa mafanikio ya Yanga hayawezi kutegemea ubora wa kikosi pekee, bali yanahitaji ushiriki wa wanachama na mashabiki kwa kujaza uwanja na kuishangilia timu.

“Hakuna YANGA BINGWA bila sisi Wanachama na Mashabiki. Kujaza Uwanja na kupaza sauti kuwashangilia wachezaji ni JUKUMU LETU,” ameandika Kamwe.

Aidha, Kamwe amewataka mashabiki kuachana na hali ya kusherehekea na kuanza kazi ya kuisaka kwa nguvu zote nafasi ya Yanga kutwaa ubingwa wa sita mfululizo.

Amesema matawi ya Yanga jijini Dar es Salaam yanapaswa kuhamasishana na kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi KMC Complex kwa lengo la kuipa timu nguvu katika kusaka pointi tatu za kwanza nyumbani.

Katika hatua nyingine, Kamwe amewakumbusha mashabiki kuwa tiketi za mchezo huo zinapatikana kupitia mfumo mpya wa ununuzi wa tiketi uliotangazwa na Bodi ya Ligi.

Pia ameeleza kuwa Idara ya Habari na Wanachama ya Yanga itaanza kutoa elimu kwa wanachama kuhusu namna ya kununua tiketi kupitia simu za mkononi, huku akiwataka wale ambao tayari wameutumia mfumo huo kuwasaidia wenzao kupata tiketi.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12:30 jioni katika Uwanja wa KMC Complex, huku Yanga ikilenga kuanza kampeni yake ya nyumbani kwa ushindi mbele ya Coastal Union.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’