Tuzo nyingine kwa Maxi Nzengeli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Aug 2026
Tuzo nyingine kwa Maxi Nzengeli

Katika mechi ya pili mfululizo jana kiungo Maxi Nzengeli aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo baada ya kuiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa KMC Complex.

Maxi alikuwa miongoni mwa wafungaji katika mchezo huo ambao Yanga ilitawala kwa dakika zote 90.

Maxi ameanza vyema msimu kwani licha ya kubeba tuzo hizo, pia amefunga bao kwenye kila mchezo akiwa miongoni mwa wachezaji wachache waliofunga mabao mawili baada ya mechi mbili.

Tangu ujio wa kocha Manqoba Mngqithi, Maxi amekuwa akitumika kama kiungo namba 8, akin'gara safu ya kiungo akishirikiana na Duke Abuya na Mudathir Yahya ambaye pia jana alifunga bao lake la kwanza msimu huu.

Licha ya mabadiliko ya makocha katika misimu mitatu, Maxi ameendelea kuwa na uhakika wa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’