Tuko asilimia 25 ya ubora wetu - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Aug 2026
Tuko asilimia 25 ya ubora wetu - Kamwe

Yanga SC imeanza vyema kampeni yake ya Ligi Kuu ya NBC, ikipata ushindi wa pili mfululizo baada ya kuichapa Coastal Union mabao 4-1 jana kwenye Uwanja wa KMC Complex. Ushindi huo umefuatia ule wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa kwanza.

Kwa mtazamo wa haraka, matokeo haya yanaweza kutoa picha kwamba Yanga tayari imeanza kutengeneza mashine ya ushindi. Lakini kwa upande wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe, Wananchi hawapaswi kuingia kwenye presha ya sifa wala kuamini kwamba timu tayari imefikia ubora wake wa juu.

Kamwe amesisitiza kuwa Yanga bado iko kwenye hatua za kujenga timu na kwa makadirio yake, kikosi hicho kwa sasa kiko karibu asilimia 25 tu ya kile ambacho benchi la ufundi linataka kukiona uwanjani.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika uhumbe huu;

"Timu yetu Bado. Tusiingie presha ya Wachambuzi na wala tusilewe sifa. Yanga Bado kufika kwenye Ubora unaosemwa au kuandikwa hivi sasa.

Kama ni asilimia ndio kwanza Tuko asilimia 25 ya Kile benchi la Ufundi inachokitaka kitokee uwanjani.

Tumpe Muda Kocha wetu Mangoba Mngqithi aendelee kuweka mambo sawa katika uwanja wa mazoezi.

Tuendelee kuwapa nguvu wachezaji wetu waendelee kujituma na kuelewa mipango ya Benchi la ufundi ili tuupate Muunganiko sahihi wa kupeleka maafa kwa wapinzani

Neno langu kwa Wananchi. Style of Play yetu mmeiona. Inahitaji wachezaji kujituma na kukimbia zaidi uwanjani.

Nataka niwahakikishie Wananchi , wakufanya jambo Hili litokee ni sisi Mashabiki. Tukija kwa wingi viwanjani, Tukashangilia na Hamasa mwanzo mwisho Mafuriko haya yatapelekwa muda wote

Jana, baada ya chuma 3 ni kama tuliridhika Majukwaani na tukaanza kuangalia mpira kwa kuchezea simu. Hii ni SUMU KUBWA. Tukipoa sisi, kila kitu kinapoa.

Ili wachezaji wetu wawe kwenye kasi ya juu muda wote wanahitaji kusikia sauti zetu. Kama Kocha anataka timu isipoe, kwanini sisi Tunapoa? Tusipoe. Hakuna kuridhika. Tutashika simu zetu mechi ikiisha.

Natumai Jumatatu In Shaa Allah, tutarekebisha Hili na Mashabiki/ Wanachama kutoka matawini Tutaishangilia Yanga yetu mwanzo mwisho."

Kauli hiyo inakuja licha ya Yanga kuonyesha ubora mkubwa dhidi ya Coastal Union, ambapo ilifunga mabao manne kupitia Albert Kangwanda, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya na Mohamed Hussein β€˜Zimbwe Jr’. Pia, Peter Shalulile alifunga mabao mawili ambayo hayakuhesabiwa baada ya kuonekana ameotea.

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’