Manqoba anataka kila mshambuliaji Yanga afunge

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Aug 2026
Manqoba anataka kila mshambuliaji Yanga afunge

Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amesisitiza umuhimu wa kila mshambuliaji wa timu hiyo kuanza kufunga mapema msimu huu, akiwataka wachezaji wake kuwa na kujiamini zaidi wanapokuwa mbele ya lango.

Mshambuliaji Peter Shalulile tayari amefungua akaunti yake ya mabao katika Ligi Kuu ya NBC, tofauti na mwenzake, Cheikh Ibrahim Toure, ambaye bado anasubiri bao lake la kwanza katika mechi za mashindano.

Hata hivyo, Toure anaweza kupata nafasi zaidi katika michezo ijayo kutokana na mkakati wa Mngqithi wa kuwapa nafasi washambuliaji wake wote ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa tayari na anabaki kuwa mshindani ndani ya kikosi.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, Mngqithi alianza na Shalulile kabla ya kumuingiza Toure kipindi cha pili. Kocha huyo pia alimtumia Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ kama winga, akieleza kuwa moja ya sababu ilikuwa kumtengenezea nafasi Toure ili aweze kufunga.

Pamoja na mpango huo, Zimbwe Jr ndiye aliyefanikiwa kuandika jina lake kwenye ubao wa mabao baada ya mpira wake wa krosi kubadilika mwelekeo na kujaa nyavuni.

“Nahitaji washambuliaji wangu wajiamini mapema sana ndani ya msimu huu. Cheikh Toure bado hajafunga, hivyo kwa upande wangu ni muhimu kuona wote wanaanza kufunga kwa sababu itawaondolea uoga na itawafanya wafocus zaidi,” alisema Mngqithi.

Yanga kesho Jumapili itarejea uwanjani katika KMC Complex kuikabili JKT Tanzania, mchezo ambao unaweza kumfanya Mngqithi aanze na washambuliaji wake wawili, Shalulile na Toure, kama alivyofanya katika mchezo wa kwanza wa msimu dhidi ya Namungo FC.

Mbali na Shalulile na Toure, Yanga pia imeongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji baada ya kukamilisha usajili wa Seleman Mwalimu kutoka Wydad AC.

Mwalimu sasa anasubiri nafasi yake ndani ya kikosi hicho baada ya Yanga kukamilisha usajili wake dakika za mwisho, wakati awali alikuwa mbioni kujiunga na Simba.

Kwa kuongezeka kwa chaguo katika safu ya ushambuliaji, Mngqithi anaonekana kutaka ushindani mkubwa ndani ya kikosi, huku kila mshambuliaji akitakiwa kutumia nafasi atakayopewa na kuthibitisha uwezo wake mbele ya lango.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’