Mashabiki wa Yanga wana shauku kubwa ya kuwaona uwanjani nyota wao wapya Stephane Aziz Ki na Seleman Mwalimu, hata hivyo unaweza kusema ni suala la muda tu watawaona.
Inaelezwa wachezaji hao wamepewa program maalum ya mazoezi ili kuwa katika uimara sahihi wa mwili 'fitness' kabla ya kuanza kutumika.
Meneja wa habari na mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa wachezaji hao hawana changamoto yoyote, muda wao utakapofika wataonekana uwanjani.
Kamwe amesema kwa sasa malengo ya Yanga ni kushinda michezo yake bila ya kujali ni mchezaji gani ameanza kikosini. Amewataka mashabiki kuendelea kuiunga mkono timu yao na kumpa sapoti kila mchezaji.
Leseni ya Mwalimu fresh
Katika hatua nyingine Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Clifford Ndimbo amethibitisha kuwa mshambuliaji Seleman Mwalimu ameidhinishwa kuwatumikia mabingwa hao wa nchi na leseni yako ilishatoka.
Kauli hiyo inafuta uvumi uliopo mitandaoni kuwa klabu ya Simba imemuwekea pingamizi mchezaji huyo wakidai kulipwa gharama binafsi walizotumia kabla ya mchezaji huyo 'kuwatoroka' na kujiunga na Yanga.
Kwa sasa kinachosubiriwa ni Mwalimu kuwa tayari kama ilivyo kwa Aziz Ki kabla ya kuanza rasmi kutumika