Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amesema kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki anaendelea kuimarika akiwa kwenye program maalum ya mazoezi kabla ya kuanza rasmi kutumika.
Kumekuwa na shauku kubwa kwa mashabiki wa Yanga kumuona Aziz Ki kwenye kikosi baada ya usajili wake kutoka klabu ya Al Ittihad ya Libya.
Manqoba amesema mchezaji huyo hakupata pre-season hivyo hawezi kuharakisha kumtumia kabla ya kuwa kwenye hali ya mchezo ili kumuepusha na majeraha.
"Aziz Ki amefikia 4/10 ya utayari wake. Hakupata pre-season hivyo ndio ameanza mazoezi sasa. Lazima tumuandae awe tayari kabla ya kuanza kumtumia kwani tunafahamu atakuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi chetu msimu huu."
"Siwezi kuharakisha kumchezesha halafu apate majeraha, hivyo sitarajii kumuona akicheza mechi mbili zinazofuata kabla ya ligi ya mabingwa," alisema Manqoba.
Akimzungumzia mshamuliaji Clement Mzize, Manqoba alisema ameendelea kuimarika na anatarajia atarejea uwanjani ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.
Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji utakaopigwa kesho Ijumaa kwenye uwanja wa KMC Complex, Manqoba amesema wanajua wanakwenda kukabiliana na timu imara kwenye ulinzi na hatari kupitia mashambulizi ya kushitukiza.
Hata hivyo wamefanya maandalizi ya kuhakikisha wanatumia vyema uwanja wa nyumbani huku akiwataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti wachezaji wao.