Wapo waliobeza uamuzi wa Yanga kujitoa kwenye michuano ya kombe la Kagame wengi wakihusisha kujitoa kwao na kuwakimbia Simba kwa kuwa walipangwa kundi moja.
Lakini moja ya sababu iliyotolewa na Yanga ya kuwapa wachezaji wake mapumziko kutokana na kukabiliwa na mashindano mengi imedhihirika baada ya timu nyingine kutangaza kutotumia vikosi vyao vya kwanza.
Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr amesema kikosi cha pili cha timu yake ndicho kitakuja nchini kushiriki michuano hiyo.
Gor Mahia itacheza na Yanga Julai 18 jijini Nairobi kwenye mchezo wa kombe la shirikisho hivyo wengi walitarajia uamuzi wao huo.
Lakini hata Simba inadaiwa kuwa na mpango wa kuwapa mapumziko wachezaji wake hivyo itatumia idadi kubwa ya wachezaji wa kikosi cha pili.
Michuano ya kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Juni 28, 2018 ni dhahiri itakosa msisimko kutokana na waandaaji wake mwaka huu kuyaibua mashindano hayo bila ya mpangilio.
Michuano hiyo itafanyika sambamba na michuano na kombe la dunia ambapo kwa hakika hakutakuwa na mahudhurio makubwa viwanjani kinyume na matarajio ya waandaaji.

ADVERTISE HERE