Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji hapo jana, hakuna muda wa kupoteza kwa Wananchi kwani leo wameelekea mkoani Arusha tayari kwa mchezo unaofuata.
Jumanne, Septemba 1 Yanga watashuka dimba la Sheikh Amri Abeid kuwakabili wenyeji wao Fountain Gate katika mchezo wa raundi ya tano.
Mabingwa hao watetezi wanakwenda Arusha wakiwa na mkakati wa kuendeleza wimbi la ushindi kwenye ligi kuu ya NBC msimu huu.
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea Botswana kuanza kampeni ya ligi ya mabingwa msimu huu ambapo mchezo wa kwanza wa hatua ya awali watacheza dhidi ya Gaborone United Septemba 06.






ADVERTISE HERE