Katika mechi nne za ligi kuu ambazo kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli ameitumikia Yanga, nyota huyo kutoka DR Congo ameondoka na tuzo tatu za nyota wa mchezo.
Jana Maxi alibeba tuzo yake ya tatu kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji akiiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Sio tuzo tu, Maxi pia amefunga kwenye mechi tatu kati ya nne, alizocheza sasa akiongoza orodha ya wafungaji kwenye kikosi cha Yanga akiwa na mabao matatu.
Ni wazi Maxi atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu kwa mwezi August 2026 na pengine anastahili kushinda tuzo hiyo.

ADVERTISE HERE