Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amewataka mashabiki wa timu hiyo mkoani Arusha kujitokeza kwa wingi uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate.
Kesho Jumatatu majira ya saa 10 jioni, Yanga watakuwa ugenini kumenyana na Fountain Gate katika dimba hilo la Sheikh Amri Abeid ukiwa ni mchezo wa raundi ya tano.
Akizungumza na wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Manqoba alisema anatambua hautakuwa mchezo mwepesi kwa kuzingatia Fountain Gate inanolewa na kocha Fredy Minziro ambaye anaifahamu vyema Yanga.
Amesema Fountain Gate licha ya kukosa ushindi kwenye mechi zilizopita, wamejipambanua kwa kuwa na timu yenye ushindani hivyo hawapaswi kuwadharau.
“Hizi ni miongoni mwa mechi ngumu na ni muhimu sana Kushinda, tunafahamu Fountain Gate wana mwalimu mzuri ambaye amewahi kuwa sehemu ya Benchi la Yanga hivyo anajua tamaduni za klabu, Ni mzoefu na ana wachezaji wazuri, Sisi kama Yanga tunapaswa kufanya kazi kubwa ili kushinda kesho”
“Tunafahamu wapinzani wetu wamepoteza michezo kadhaa hapo nyuma lakini jukumu letu ni kuheshimu kila mchezo, tumewaangalia Fountain Gate namna wanavyocheza na leo tunakwenda kufanya maandalizi ya mwisho ya kucheza nao, naamini tutakuwa na Mechi nzuri”
“Nawaomba sana Wananchi waje kwa Wingi, wao ni muhimu sana kwa timu, ni muhimu pia Kwangu kama kocha kwasababu wananipa morali ya kufanya vyema kila siku, nawashukuru sana kwa sapoti yao tangu tumefika hapa nchini na nawaomba kesho waje ili tushinde pamoja,” alisema Manqoba