Baada ya mpango wa kutua Yanga kukwama, Mabula aibukia JS Kabylie

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Sep 2026
Baada ya mpango wa kutua Yanga kukwama, Mabula aibukia JS Kabylie

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Alphonce Mabula Msanga, hatimaye ameibukia katika klabu ya JS Kabylie ya Algeria, baada ya kuhusishwa kwa nguvu na mabingwa wa Tanzania, Yanga SC, katika dirisha lililopita la usajili.

Mabula, mwenye umri wa miaka 23, amejiunga na JS Kabylie kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Shamaxi FK ya Azerbaijan mwishoni mwa Juni 2026.

Taarifa kutoka Algeria zinaeleza kuwa amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Tizi Ouzou.

Usajili huo ulikamilika katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili nchini Algeria, huku JS Kabylie ikifanikiwa kuipita klabu nyingine zilizokuwa zikimuwania kiungo huyo.

Yanga ilimtaka Mabula

Kabla ya kuibukia Algeria, jina la Mabula lilikuwa gumzo kwenye dirisha la usajili nchini Tanzania baada ya Yanga kuanza mazungumzo ya kumrudisha nyumbani.

Iliripotiwa mwezi Julai kwamba Yanga ilikuwa imeanza mazungumzo na Mabula, ikiwa na lengo la kumuongeza katika eneo la kiungo mkabaji. Wakati huo Mabula alikuwa amemaliza mkataba wake na Shamaxi na alikuwa mchezaji huru.

Baadaye, taarifa zikaeleza kuwa mazungumzo ya awali yalifikia makubaliano lakini mchezaji huyo hakusaini mkataba kwa wakati kwa kuwa alikuwa akisikilizia ofa nyingine alizokuwa nazo.

hatimaye Yanga ikamsajili kiungo Fredy ngoma na kufuta rasmi mpango wa kumsajili kiungo huyo huku pia Yanga ikikamilisha hesabu zake za usajili kwa kumrejesha Stephane Aziz Ki siku chache kabla ya dirisha kufungwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’