Jana mashabiki wa Yanga walimshuhudia beki Farouk Komara kwa mara ya kwanza akicheza dakika 90 tangu aliposajiliwa na Wananchi kwenye dirisha lililopita.
Komara alianza safu ya beki wa kati sambamba na Ibrahim Bacca akionyesha uwezo mkubwa hasa kwenye upigaji pasi na kucheza mipira ya juu.
Kulikuwa na shaka juu ya uwezo wa beki huyo raia wa Ivory Coast ambaye alijiunga na Yanga akitokea klabu ya Golden Arrows ya Afrika Kusini.
Lakini ni wazi dakika zake 90 kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate zimewathibitishia Wananchi kuwa wamepata mchezaji.
Komara sio tu anaweza kucheza beki wa kati, nyota huyo pia anaweza kutumika kama kiung mkabaji.
ADVERTISE HERE