Job, Mzize wajumuishwa safari ya Botswana, waishia Afrika Kusini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Sep 2026
Job, Mzize wajumuishwa safari ya Botswana, waishia Afrika Kusini

Nyota wa Yanga Clement Mzize na Dickson Job wamejumuishwa kwenye msafara wa kikosi cha Yanga kilichoondoka mapema leo jijini Dar es salaam kuelekea Botswana tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United.

Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Septemba 05 huko Gaborone, saa 2 usiku kwa saa za Tanzania.

Baada ya kikosi cha Yanga kuwasili Johannesburg Afrika Kusini kuunganisha ndege ya kuelekea Botswana, Mzize na Job wao wamesalia Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa Mzize na Job watafanyiwa uchunguzi kubaini kama wamepona majeraha yaliyowaweka nje kwa muda mrefu.

"Kabla ya wachezaji hao kurejea kwenye majukumu yao lazima tujiridhishe kama wamepona sawa sawa ili isije kutokea ikawa wamewahishwa kurejea uwanjani kabla ya kupona sawasawa," alisema Kamwe.

Nyota hao wamerejea kwenye hospitali ambayo walifanyiwa upasuaji awali na endapo itabainika wamepona sawasawa, huenda wakashuhudiwa kikosini karibun

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’