Kikosi cha Yanga kimewasili salama Gaborone huko Botswana tayari kwa mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United. Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Septemba 05.
Yanga imetua Botswana ikiwa na kikosi cha wachezaji 28 ambao wanakwenda kuipambania nembo ya Yanga kwenye mchezo huo wa ugenini.
Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amepania kumaliza mchezo huo ugenini na kurejea Dar kukamilisha hesabu wiki ijayo.
Yanga itakuwa na takribani siku tatu za kukamilisha maandalizi hapo Gaborone tayari kuwakabiliwa wapinzani wao Jumamosi.






ADVERTISE HERE