Manji ni suluhu ya muda mfupi ya matatizo ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2018
Manji ni suluhu ya muda mfupi ya matatizo ya Yanga
Uamuzi wa mfanyabiashara Yusuph Manji kurejea kwenye nafasi ya uenyekiti Yanga unatajwa kama suluhisho la muda mfupi la kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili klabu hiyo.

Tangu Manji alipotangaza kujiweka kando katika nafasi hiyo mwezi Mei mwaka jana, Yanga imekuwa ikipita katika milima na mabonde ambayo idadi kubwa ya wadau wa soka wamekuwa wakiihusisha moja kwa moja na kukosekana kwake klabuni.

Kabla ya kuanza kwa msimu uliomalizika, Yanga ilijikuta ikiwa na deni linalotajwa kuwa zaidi ya Sh200 milioni, ambalo lilitokana na madai ya posho na mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi katika kikosi chake ambacho kilitetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo

Wakati wa usajili wa msimu uliomalizika Yanga iliwapoteza wachezaji wake muhimu kama Vincent Bossou, Deus Kaseke na Haruna Niyonzima ambao walitimka baada ya kushindwa kuafikiana dau la kuongeza kusaini mikataba mipya baada ya ile ya awali kumalizika.

Lakini pia iliwakosa baadhi ya nyota wapya iliyotegemea kuwasajili kutokana na kuzidiwa kete na baadhi ya timu pinzani.

Mbali na hilo, Yanga ililazimika kutofanya usajili mkubwa huku ikitumia fedha kiduchu katika dirisha kubwa la usajili tofauti na ilivyokuwa ikifanya miaka ya nyuma.

Jinamizi hilo liliendelea kuisumbua Yanga katika ligi, na kupelekea imalize kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC na Simba iliyotwaa ubingwa.

Yanga pia ilitolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la FA (ASFC) hivyo kupelekea ikose nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao

Moja ya mambo yanayodaiwa kusababisha Yanga 'kuboronga' msimu uliomalizika ni pamoja na kupungua morali kwa wachezaji wake kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.

Kwa hali ilivyo wakati huu ni dhahiri hakuna mtu anayeweza kumaliza matatizo na changamoto zote zinazoikabili Yanga zaidi ya Manji.

Hivyo lilikuwa jambo la busara kwa wanachama kupitia Mkutano Mkuu kukataa kujiuzulu kwake na kumuomba arejee klabuni ili airudishe Yanga kwenye mstari.

Yanga inalazimika kuweka mambo yake sawa kabla ya haijaingia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji ambao tayari umeridhiwa na kuwekwa kwenye katiba ya klabu hiyo.

Wakati huu Yanga imeunda Kamati Maalum ya Mpito inayotafuta fedha kwa ajili ya kusajili wachezaji pamoja na kushughulikia mikataba ya wachezaji iliyomalizika.

Tayari Manji amepelekewa taarifa ya maazimio ya Wanachama ya kukataa barua yake ya kujiuzulu na kumuomba arejee kwenye nafasi yake.

Licha ya ukimya wake tangu kupelekewa maazimio hayo, kumekuwa na taarifa kuwa Manji amekubali kurejea na amekuwa akishirikiana na Kamati iliyoundwa na Bodi ya Wadhamini katika masuala ya usajili.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’