Mpya

Aziz Ki apunguziwa presha Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10h ago
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga

Licha ya mashabiki wa Yanga kutamani kumuona kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki pengine akianza kila mchezo, Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amesisitiza kuwa nyota huyo bado hajafikia utimamu wa mwili wa asilimia 100 kuweza kucheza dakika 90.

Kwenye mchezo uliopita wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United, Aziz Ki alitumika kwa dakika 45 za kipindi cha pili huku akiwekwa kwenye ulinzi mkali na wachezaji wa Gaborone ambao walihakikisha wanakuwa wengi kumdhibiti kila alipogusa mpira.

Manqoba amesisitiza kuwa Aziz Ki ataendelea kucheza dakika 45 hadi 60 kwa wakati huu ambao anaendelea kuimarika huku akisisitiza kuwa nyota huyo ni mchezaji muhimu katika mipango ya Yanga hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa (CAFCL).

"Kwa sasa fitness yake imeongezeka tofauti na alipojiunga nasi, nitaendelea kumpa dakika za kucheza ili awe timamu zaidi. Bado sifikirii kumpa zaidi ya dakika 60 kwani bado hajafikia kwenye kiwango cha utimamu anachopaswa kuwa. "

"Aziz Ki ni mtu muhimu sana kiufundi na ataongeza thamani kubwa kwenye kikosi chetu pale atakapokuwa fit kwa asilimia 100," alisema Manqoba

Baada ya kutoanza mchezo uliopita, kuna uwezekano mkubwa Manqoba akamuanzisha Aziz Ki kesho kwenye mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United

More Stories

Maandalizi ya kuikabili Gaborone United yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Gaborone United yamekamilika
10m ago
READ MORE β†’
Toure anajiamini, atafunga sana
Toure anajiamini, atafunga sana
4h ago
READ MORE β†’
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
7h ago
READ MORE β†’
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY
7h ago
READ MORE β†’
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
7h ago
READ MORE β†’
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
14h ago
READ MORE β†’
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’