Mpya

Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7h ago
Mwalimu awaalika Wananchi SELE DAY

Mshambuliaji wa Yanga Seleman Mwalimu 'Gomez' amewaalika mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa winga uwanja wa Azam Complex hapo kesho katika mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) dhidi ya Gaborone United.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Mwalimu alisema ni heshima kubwa kwake kuwa sehemu ya wachezaji wanaokwenda kuipambania nembo ya Yanga katika mchezo huo.

Amesema wachezaji wote wako tayari na wanaichukulia mechi hii kwa uzito mkubwa kwa sababu imebeba hatma yao ya kufuzu raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa.

Licha ya kutambua ugumu wa mchezo huo, Mwalimu amesema wamekuwa na wakati mzuri wa maandalizi kwenye uwanja wa mazoezi akiamini kwenye uwezo wa benchi la ufundi chini ya kocha Manqoba Mngqithi katika kuwasoma wapinzani na hivyo wataingia kwenye mchezo huo na mbinu sahihi zitakazowahakikishia ushindi.

“Tunaichukulia mechi hii kwa ukubwa wake, kwa sababu ni mechi yenye hatma yetu kimataifa msimu huu. Benchi letu la ufundi limefanya kazi kubwa kuhakikisha tunatengeneza mipango bora. Tumejipanga vizuri kuhakikish tunapata ushindi. Malengo yetu ni kuhakikisha tunafika mbali katika michuano hii ya Kimataifa.”

“Yanga kwa sasa tuna kocha mkubwa. Tayari ameona ubora na udhaifu wa mpinzani. Kwenye kiwanja cha mazoezi mwalimu na benchi lake la ufundi wametuelekeza namna ya kucheza na wapinzani wetu. Presha ambayo tumepeleka Botswana tutaipeleka hapa mara mbili. Nina matumaini kabla ya kipindi cha pili tutakuwa na matokeo sahihi”

“Nina washukuru viongozi na mashabiki kwa kuandaa mchezo huu kupitia jina langu. Ninafarijika sana kuona klabu inatambua mchango wangu. Kwangu hili ni deni kubwa ambalo napaswa kulipa. Timu ina wachezaji wengi lakini ukiona wameita mechi kwa jina lako basi ujue kuna heshimu kubwa sana unapata kutoka kwa hao watu. Niwahakikishie tutajitoa kwa zaidi ya asilimia 100,” alisema Mwalimu

More Stories

Maandalizi ya kuikabili Gaborone United yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Gaborone United yamekamilika
9m ago
READ MORE β†’
Toure anajiamini, atafunga sana
Toure anajiamini, atafunga sana
4h ago
READ MORE β†’
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
Manqoba aondoka na tuzo ya ligi kuu August
7h ago
READ MORE β†’
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
Hatutawadharau Gaborone United - Manqoba
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
Aziz Ki apunguziwa presha Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
Sele Day tiketi zinaelekea ukingoni
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
Manqoba na ndoto ya fainali ligi ya mabingwa
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
14h ago
READ MORE β†’
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
Pacome aongoza hamasa KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’