Usajili upi 'utabamba' Yanga?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jun 2018
Usajili upi 'utabamba' Yanga?
Ifahamike Yanga bado haijaweka hadharani wachezaji iliyowasajili msimu huu.

Kwa pamoja Kamati ya mpito inayoongozwa na Abbasi Tarimba, Kamati ya Mashindano na ile ya usajili ambazo zote zinaongozwa na Hussein Nyika wamekubaliana kuendelea na utaratibu huo wa kusajili kimyakimya na kuweka mambo hadharani baada ya zoezi zima la usajili kukamilika.

Licha ya mambo kupelekwa kimyakimya, tetesi za baadhi ya wachezaji wanaotajwa kutua Yanga zimekuwa zikiwekwa hadharani na vyombo mbalimbali vya habari.

Baadhi ya wachezaji wamekiri kuwa kwenye mazungumzo na Yanga huku wengine wakibainisha kuwa wameshamalizana, wanasubiri kusaini.

Hapa tumeweka orodha ya baadhi ya wachezaji ambao huenda wakatua Jangwani baada ya maamuzi ya mwisho kufikiwa na uongozi wa Yanga.

1. Marcelin Koukpo

Huyu ni mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Benin. Ana umri wa miaka 23, aliwasili nchini wiki iliyopita na kupokelewa na Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten.

Baada ya kutimka kwa mshambuliaji Obrey Chirwa, hakuna shaka juu ya usajili wa Koukpo.

Mpaka wakati huu bado yuko nchini na anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoanza kujifua na kikosi cha Yanga hivi karibuni

2. Serge Wawa

Mkataba wa Wawa na klabu ya Al Hilal umemalizika na kwa nyakati tofauti mwenyewe alikiri kufikia makubaliano na uongozi wa Yanga.

Yanga imedhamiria kusajili beki wa kati mzoefu. Wawa ameitumikia klabu ya Azam FC kwa mafanikio makubwa msimu 2013/14 na 2014/15 kabla hajarejea kwenye klabu yake ya zamani ya Al Hilal.

Ujio wake Yanga utakuwa ni habari njema kwa safu ya ulinzi kwani utaimarisha safu hiyo ambayo msimu uliomalizika uliwategemea zaidi Kelvin Yondani na Andrew Vicent.

3. Vumi Ley Matampi/Farouk Shakalo/Benedict Tinocco

Hawa ni walinda mlango ambao mmoja wapo huenda akatua Yanga kurithi mikoba ya Youthe Rostand.

Matampi aliyemaliza mkataba kwenye klabu ya TP Mazembe alipendekezwa na kocha Mwinyi Zahera.

Zahera amekutana na Matampi katika kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo.

Shakalo anatokea Kenya kwenye klabu ya Bandari akidaiwa kupendekezwa na Razack Siwa anayetarajiwa kuwa kocha mpya wa makipa wa Yanga.

Tinnoco amekipiga katika klabu ya Mtibwa Sugar msimu uliomalizika. Kiwango chake kimezivutia timu nyingi ikiwemo Yanga.

Hivi karibuni mlinda lango huyo ambaye alitua Mtibwa Sugar baada ya kuachwa na Yanga, alikiri mabosi wake hao wa zamani kutaka kumrejesha kundini.

Hata hivyo Yanga inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Singida United ambayo inasaka mlinda lango baada ya kutokea sintofahamu na mlinda lango wao Manyika Peter Jr anayetaka kuvunja mkataba.

4. Laudirt Mavugo

Mavugo amekiri kuwa katika mazungumzo na uongozi wa Yanga hivi karibuni. Mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Burundi, amegoma kusaini mkataba wa mwaka mmoja, ofa aliyopewa na timu yake ya sasa, Simba.

5. Said Khamis Ndemla

Ndemla siku za hivi karibuni ameandikwa sana na vyombo vha habari akidaiwa kugoma kuhuisha mkataba wake na klabu ya Simba.

Ndemla ni mchezaji huru, naye amekiri kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga. Ibrahim Ajib aliyetua Yanga kutoka Simba msimu uliomalizika, anatajwa kumshawishi Ndemla akubali ofa ya Yanga.

6. Francis Kahata/ Meddy Kagere

Alianza Meddy Kagere kuhusishwa na Yanga halafu akafuata Francis Kahata. Hata hivyo uongozi wa Yanga umekanusha kuwafuatilia wachezaji hao.

7. Felly Mulumba

Huyu ni Mcongo, mchezaji kiraka kutoka klabu ya Bandari ya Kenya. Mulumba ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji na nafasi zote za ulinzi wa kati.

Mulumba huenda akawa miongoni mwa wachezaji wa mwanzo kabisa kutangazwa kusajiliwa na Yanga.

8. Djako Arafat

Arafat alikuwa mshambuliaji wa kwanza kabisa kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga na kufikia makubaliano.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika alikiri kumalizana na mshambuliaji huyo na alikuwa akisubiri baraka za kocha Mwinyi Zahera ili aweze kusajiliwa.

9. Mrisho Ngassa

Ngassa hakuna shaka juu ya kurejea kwake Jangwani. Ni miongoni mwa wachezaji wa kwanza kabisa kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga muda mfupi baada ya ligi kumalizika.

Juzi Mzee Khalfan Ngassa, baba yake mzazi Mrisho, alipongeza uamuzi wa mwanawe kurejea Yanga na kumtabiria kuwa ataweza kurejesha makali yake kwa kuwa atakuwa akicheza klabu ya ndoto yake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’