Mpya

Mabao saba wamehusika washambuliaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2d ago
Mabao saba wamehusika washambuliaji Yanga

Mechi mbili za hatua ya awali ligi ya mabingwa zimekamilika huku Yanga ikifanikiwa kutinga raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 dhidi ya Gaborone United.

Kilichowafurahisha mashabiki wa Yanga ni kuona washambuliaji wao wote watatu wanashiriki katika kuivusha Yanga kufuzu raundi ya kwanza.

Seleman Mwalimu ndiye aliyefunga bao la kusawazisha dakika za lala salama kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Botswana na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.

Peter Shalulile juzi akaitanguliza Yanga kwa kufunga bao la kwanza dimba la Azam Complex akipokea pasi kutoka kwa Mwalimu kabla ya Cheick Ibrahim Toure kuongeza bao la pili kipindi cha pili.

Pengine Mwalimu angeweza kufunga tena katika mchezo huo lakini pasi yake ya bao ilikuwa muhimu.

Mpaka sasa washambuliaji wa Yanga wamehusika kwenye mabao 7 katika mashindano yote.

Shalulile anaongoza akiwa amefunga mabao manne (matatu kafunga kwenye ligi), Toure amefunga mabao mawili (moja kwenye ligi) na Mwalimu amepachika bao moja kwenye ligi ya mabingwa

More Stories

Wachezaji wetu wameonyesha tabia ya kibingwa - Kamwe
Wachezaji wetu wameonyesha tabia ya kibingwa - Kamwe
44m ago
READ MORE β†’
Mzize 'amkosha' Manqoba
Mzize 'amkosha' Manqoba
3h ago
READ MORE β†’
Highlights; Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
Highlights; Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL
FT : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL
15h ago
READ MORE β†’
Goal : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
Goal : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Geita Gold, NBC PL, Sept 15
Kikosi : Yanga vs Geita Gold, NBC PL, Sept 15
19h ago
READ MORE β†’
Mzize kurejea dhidi ya Geita Gold leo
Mzize kurejea dhidi ya Geita Gold leo
21h ago
READ MORE β†’
Shalulile hatihati kuikosa Geita Gold
Shalulile hatihati kuikosa Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’
Casemiro, Chuga Boy katika majukumu ya timu ya Taifa U20
Casemiro, Chuga Boy katika majukumu ya timu ya Taifa U20
1d ago
READ MORE β†’