Mlinzi wa Yanga Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema wamedhamira kuchukua alama tatu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa KMC Complex.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Zimbwe Jr amesema licha ya ufinyu wa muda wa maandalizi, lakini anaamini mazoezi waliyofanya kwa siku mbili yatawaweka katika nafasi nzuri ya kuikabili Geita Gold.
Aidha Zimbwe Jr amekiri kuwa Geita Gold ni timu nzuri yenye wachezaji wenye uzoefu hivyo wanatarajia mchezo hautakuwa mwepesi.
“Kama timu tunaendelea vizuri kwa ajili ya mchezo wa kesho. Ni kweli hatukuwa na muda mrefu wa kufanya maandalizi makubwa, lakini tunaamini maandalizi ya jana na leo yatatusaidia kuwa tayari kwa mchezo.”
“Geita Gold ni timu nzuri. Tumefuatilia baadhi ya michezo yao na tumeona wana wachezaji wazuri ambao mmoja mmoja wanafanya vizuri, lakini kwa ujumla pia ni timu yenye ubora. Tumemchambua mpinzani wetu kwa ukaribu. Tumebaini baadhi ya nguvu na mapungufu yao, hivyo tunakwenda kuyafanyia kazi ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo wa kesho,” alisema