Mpya

Matchday: Yanga vs Geita Gold, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1d ago
Matchday: Yanga vs Geita Gold, NBC PL

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC, Yanga Sc leo wanarudi kwenye kampeni ya kurejesha taji hilo Jangwani kwa msimu wa sita mfululizo pale watakapo wakaribisha Geita Gold katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex, saa 1 usiku.

Baada ya kufanikiwa kuvuka hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa, 'focus' ya Wananchi sasa imerudi kwenye ligi.

Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, Wananchi watashuka KMC Complex kuzisaka alama tatu muhimu ambazo zitawahakikishia kuendelea kusalia kileleni kabla kukutana na watani zao Simba kwenye mchezo unaofuata baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

Akizungumza na wanahabari jana, Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi aliweka bayana kuwa Geita Gold sio timu nyepesi na anatarajia kukutana na upinzani mkali.

Hata hivyo Mngqithi alisisitiza kuwa kikosi chake kiko tayari kwa ushindani wa aina yoyote wakihitaji kushinda na kusalia katika nafasi yao.

Yanga imeanza msimu huu kibabe ikiwa na rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 baada ya kushinda mechi zote za tano za kwanza.

Leo watakuwa na nafasi ya kuendeleza rekodi hiyo kwenye uwanja wa nyumbani.

More Stories

Wachezaji wetu wameonyesha tabia ya kibingwa - Kamwe
Wachezaji wetu wameonyesha tabia ya kibingwa - Kamwe
44m ago
READ MORE β†’
Mzize 'amkosha' Manqoba
Mzize 'amkosha' Manqoba
3h ago
READ MORE β†’
Highlights; Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
Highlights; Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL
FT : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL
15h ago
READ MORE β†’
Goal : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
Goal : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Geita Gold, NBC PL, Sept 15
Kikosi : Yanga vs Geita Gold, NBC PL, Sept 15
19h ago
READ MORE β†’
Mzize kurejea dhidi ya Geita Gold leo
Mzize kurejea dhidi ya Geita Gold leo
21h ago
READ MORE β†’
Shalulile hatihati kuikosa Geita Gold
Shalulile hatihati kuikosa Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’
Casemiro, Chuga Boy katika majukumu ya timu ya Taifa U20
Casemiro, Chuga Boy katika majukumu ya timu ya Taifa U20
1d ago
READ MORE β†’