Wachezaji wa Yanga Juma Abushir 'Chuga Boy' na Abdulnassir Mohamed 'Casemiro' ni sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya vijana U20 Ngorongoro Heroes ambacho kitashuka dimbani kuwakabili Rwanda.
Ni katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon U20 kwa ukanda wa CECAFA.
Mchezo huo utapigwa saa 2 usiku kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Wakati vijana hao wakishuka dimba la Uhuru kwenye majukumu ya timu ya Taifa, kaka zao watakuwa dimba la KMC Complex kuikabili Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
