Mpya

Shalulile hatihati kuikosa Geita Gold

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1d ago
Shalulile hatihati kuikosa Geita Gold

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe, amethibitisha kuwa mshambuliaji raia wa Namibia Peter Shalulile alipata jeraha katika mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Gaborone United uliopigwa mwishoni mwa wiki.

Shalulile alifunga moja ya mabao ya Yanga katika ushindi wa mabao 2-1 ambao ulitosha kuwapeleka Wananchi raundi ya kwanza ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.

Katika mchezo huo, kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi alimtoa Shalulile mwanzoni mwa kipindi cha pili nafasi yake ikichukuliwa na Albert Kangwanda.

Kamwe amesema hali ya nyota huyo bado haijakaa sawa kwa asilimia 100 na pengine anaweza kukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold utakaochezwa hii leo majira ya saa 1 usiku uwanja wa KMC Complex.

Hata hivyo washambuliaji wengine kama Seleman Mwalimu na Cheick Ibrahim Toure wako kamili na tayari kuendeleza makali ya safu ya ushambuliaji ya Yanga ambao imefunga mabao 15 katika mechi tano za ligi mpaka sasa.

More Stories

Wachezaji wetu wameonyesha tabia ya kibingwa - Kamwe
Wachezaji wetu wameonyesha tabia ya kibingwa - Kamwe
44m ago
READ MORE β†’
Mzize 'amkosha' Manqoba
Mzize 'amkosha' Manqoba
3h ago
READ MORE β†’
Highlights; Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
Highlights; Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL
FT : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL
15h ago
READ MORE β†’
Goal : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
Goal : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Geita Gold, NBC PL, Sept 15
Kikosi : Yanga vs Geita Gold, NBC PL, Sept 15
19h ago
READ MORE β†’
Mzize kurejea dhidi ya Geita Gold leo
Mzize kurejea dhidi ya Geita Gold leo
21h ago
READ MORE β†’
Casemiro, Chuga Boy katika majukumu ya timu ya Taifa U20
Casemiro, Chuga Boy katika majukumu ya timu ya Taifa U20
1d ago
READ MORE β†’