Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex jijini Dar es salaam.
Unaweza kusema ushindi ndio matokeo muhimu kwa Wananchi katika mchezo ambao Yanga ililazimika kucheza pungufu kwa zaidi ya dakika 75 baada ya Stephane Aziz Ki kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Licha ya kuwa pungufu, Yanga ilitawala kwa muda mwingi wakijipatia bao pekee la ushindi mapema kwenye kipindi cha pili likifungwa na Farouk Komara kwa kichwa.
Bado Yanga inakosa umakini eneo la mwisho kwani Seleman Mwalimu, Hussein Zakouane na hata Clement Mzize aliyeingia kipindi cha pili walikuwa karibu kufunga.
Dakika 10 za mwisho zilikuwa ngumu kwa Yanga ambapo baada ya kucheza pungufu kwa muda mrefu uchovu ilionekana kuwakabili wachezaji na kuwapa nafasi Geita Gold kutawala mchezo.
Licha ya kosakosa nyingi, Geita Gold hawakuweza kusawazisha bao hilo Yanga ikiondoka na alama zote tatu na kuendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 kwenye ligi.
Wananchi wameendelea kusalia kileleni wakifikisha alama 18 baada ya mechi 6.