Uongozi wa Yanga umesema wiki ijayo, timu hiyo inatarajiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia.
Yanga itaikabili Gor Mahia Julai 18, 2018 nchini Kenya katika mchezo wa tatu wa kombe la Shirikisho kabla ya timu hizo kurudiana Julai 29 jijini Dar es salaam.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki hii akitokea mapumzikoni Ufaransa.
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema wanatarajia wachezaji wote waliokuwa likizo mikoani kurejea jijini Dar es salaam wiki hii tayari kwa kuanza mazoezi Jumatatu, Juni 25 2018.
Mazoezi hayo yatahusisha wachezaji wapya waliosajiliwa na wale ambao watakuwa wakifanyiwa majaribio kabla ya kusaini mikataba.

ADVERTISE HERE