Mpya

Mzize 'amkosha' Manqoba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3h ago
Mzize 'amkosha' Manqoba

Jana Yanga ilifanikiwa kuendeleza kasi yake kwenye ligi kuu msimu huu wakiichapa Geita Gold bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.

Katika mchezo huo mashabiki wa Yanga walimshuhudia mshambuliaj Clement Mzize akirejea kikosini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi 7.

Akizungumza baada ya mchezo, Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi alieleza kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji huyo akibainisha wazi kuwa Mzize ni mmoja wa wachezaji wake muhimu msimu huu.

Manqoba amesema kama mshambuliaji huyo atakuwa fit haraka ni wazi atakuwa msaada mkubwa kwa Yanga msimu huu.

"Mzize amecheza vizuri sana, licha ya kuwa amerejea baada ya kukaa nje kwa takribani miezi saba. Nii miongoni mwa wachezaji muhimu katika mipango yetu msimu huu, natamani aendelee kuwa fiti," alisema Manqoba.

Mngqithi pia alibainisha kuwa beki Dickson Job nae anakaribia kurejea uwanjani huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na kikosi kamili na wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri ya utimamu wa mwili.

Katika hatua nyingine Manqoba ametetea uamuzi wake wa kufanya 'rotation' ya kikosi akisisitiza umuhimu wa kuwapa mapumziko wachezaji waliotumika zaidi ili kuwaepusha na changamoto za majeraha.

Katika mchezo huo Mngqithi hakuwatumia kabisa Yao Kouassi, Chadrack Boka, Bakari Mwamnyeto, Albert Kangwanda na Peter Shalulile ambaye ilielezwa alipata majeraha ya nyonga kwenye mchezo uliopita wa ligi ya mabingwa.

More Stories

Wachezaji wetu wameonyesha tabia ya kibingwa - Kamwe
Wachezaji wetu wameonyesha tabia ya kibingwa - Kamwe
43m ago
READ MORE β†’
Highlights; Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
Highlights; Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL
FT : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL
15h ago
READ MORE β†’
Goal : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
Goal : Yanga 1-0 Geita Gold, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Geita Gold, NBC PL, Sept 15
Kikosi : Yanga vs Geita Gold, NBC PL, Sept 15
19h ago
READ MORE β†’
Mzize kurejea dhidi ya Geita Gold leo
Mzize kurejea dhidi ya Geita Gold leo
21h ago
READ MORE β†’
Shalulile hatihati kuikosa Geita Gold
Shalulile hatihati kuikosa Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’
Casemiro, Chuga Boy katika majukumu ya timu ya Taifa U20
Casemiro, Chuga Boy katika majukumu ya timu ya Taifa U20
1d ago
READ MORE β†’