Ni kipigo kingine kwa kinadada wa Yanga Princess mbele ya Simba Queens leo wakichapwa mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii.
Sio matokeo mageni kwa kinadada wa Yanga Princess ambao kwa misimu ya karibuni wamekuwa na wakati mgumu kupata ushindi mbele ya wapinzani wao wa jadi.
Bado unaweza kusema Yanga Princess inaendelea kusukwa, matokeo haya yanatoa nafasi kwa benchi la ufundi chini ya Kocha Edna Lema kufanya maboresho muhimu kabla ya mikiki mikiki ya ligi kuu ya Wanawake kuanza.
Kipigo hicho pia kimechagizwa zaidi na kadi nyekundu ambayo Yanga Princess walipata mapema kwenye kipindi cha kwanza, nahodha Retisia Nabbosa akitolewa nje.
Kwa matokeo hayo ni wazi Edna Lema na benchi lake la ufundi wana kazi ya kufanya ili kuhakikisha angalau msimu huu Yanga Princess inawapa furaha mashabiki wa Yanga.
Tangu kuanzishwa kwa timu hii haijawahi kutwaa taji la ligi kuu ya Wanawake