Uongozi wa Yanga umewashukuru Wananchama na Mashabiki wa timu hiyo kwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru hapo jana kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Simba.
Licha ya kupoteza mchezo huo kwa mabao 2-1, Yanga imetambua thamani ya mashabiki wake ambao walijitokeza kuiunga mkono timu yao. Uongozi umewaahidi mashabiki kuwa timu yao itarejea ikiwa imara zaidi.
Baada ya mchezo huo, mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kwa misimu mitano mfululizo, wanaelekeza nguvu zao kwenye ligi ya mabingwa ambapo mchezo unaofuata ni dhidi ya CFFA ya Madagascar.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi, unatarajiwa kupigwa uwanja wa Azam Complex, Jumamosi Oktoba 17
ADVERTISE HERE