Mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya TRA United dhidi ya Yanga ambao awali ulipangwa kupigwa Oktob 13, sasa umepangiwa tarehe nyingine, Oktoba 24.
Mbele yake Yanga sasa inakabiliwa na mechi mbili za kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya CFFA ya Madagascar mechi zote zikitarajiwa kupigwa uwanja wa Azam Complex.
Mchezo wa kwanza utapigwa Oktoba 17 na mchezo wa marudio kupigwa Oktoba 21.
Baada ya mechi hizo, Wananchi watasafiri Arusha kuikabili TRA United Oktoba 24 na kisha kurejea jijini Dar es salaam kuikabili Mashujaa Fc Oktoba 27.

ADVERTISE HERE