Dida anaweza kurejea Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jun 2018
Dida anaweza kurejea Jangwani
Upo uwezekano mkubwa mlinda lango wa zamani wa Yanga Deogratius Munishi 'Dida' akarejea katika timu hiyo inayosaka kipa kwa udi na uvumba.

Msimu uliomalizika Dida aliichezea timu ya Chuo Kikuu cha Pretoria, inayofahamika kwa jina la Tuks FC ya Afrika Kusini ambayo inashiriki katika Ligi Daraja la Kwanza.

Kamati ya usajili ya Yanga inayoongozwa na Hussein Nyika inaweza 'kubadili gia angani' na kumrejesha kipa huyo kama itashindwa kunasa moja ya sahihi za makipa watatu inaowawania.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo amesema mbali na kufanya mazungumzo na makipa wa timu za nje ya Tanzania, pia wanafikiria uwezekano wa kumrejesha Dida.

"Tunataka kukamilisha kila kitu ndipo tuwatangaze tuliowasajili, suala la kipa bado kamati inaendelea kumsaka kipa mwenye ubora, ila pia tunamfikiria Dida kuweza kumleta kikosini."

Dida na Ali Mustafa 'Barthez' ndio walioisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa misimu mitatu mfululizo yaani 2015, 2016 na 2017.

Kuondoka kwao msimu uliopita kwa kiasi kikubwa kumeifanya Yanga ikose utulivu langoni baada ya Mcameroon Youthe Rostand aliyesajiliwa kushindwa kufikia matarajio.

Wakati huu Kamati ya Usajili ya Yanga iliyoongezewa nguvu na Kamati Maalum ya Abbas Tarimba, iko 'busy' kuhakikisha inakamilisha usajili kabla ya kuanza maandalizi ya kombe la Shirikisho.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’