Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye alikuwa mapumziko nchini Ufaransa amerejea usiku wa kuamkia leo, imefahamika.
Awali ilitaarifiwa kuwa kocha huyo angewasili kesho Jumammosi tayari kukiongoza kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kuanza mazoezi Jumatatu, Juni 25.
Jana wakati akihojiwa na moja ya redio maarufu nchini, Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika alisema kocha huyo alikuwa njiani na alitarajiwa kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere usiku wa kuamkia leo.
Kurejea kwa Zahera kutawezesha kukamilika kwa usajili wa wachezaji wa Kimataifa ambao alidaiwa kuuzuia mpaka arudi.
Habari njema zaidi ni kwamba Zahera ametua nchini na mshambuliaji ambaye huenda akasajiliwa kuchukua nafasi ya Obrey Chirwa aliyetimkia Misri.
Yanga bado 'imeficha' michakato yake ya usajili uongozi wa timu hiyo ukiahidi kuweka mambo hadharani baada ya zoezi zima kukamilika

ADVERTISE HERE