Kangwanda alihitaji dakika 15 kudhihirisha ubora wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29m ago
Kangwanda alihitaji dakika 15 kudhihirisha ubora wake

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Albert Kangwanda jana hakuanza vizuri mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CFFA akipoteza umakini na kuinyima Yanga mabao ya mapema kipindi cha kwanza.

Kangwanda aliibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya mashabiki wakiona kama haipambanii nembo ya Yanga kwa asilimia 100.

Hata hivyo mchezaji huyo ni kama hata mwenyewe alifahamu hakucheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushind wa mabao 4-0.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amefichua baada ya wachezaji kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko, Kangwanda alimuomba kocha Manqoba Mngqithi asimtoe, akiomba angalau dakika 15 ili akasahihishe makosa yake.

Hicho ndicho alichofanya MVP huyo wa ligi kuu ya Zambia msimu uliopita kwani dakika 15 za kipindi cha pili alizitumia ipasavyo akifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao na kuihakikishia Yanga ushindi huo mnono wa mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya hatua ya makundi CAFCL.

Hata hivyo Kangwanda alishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kupata majeraha.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ipo namna Manqoba anafelishwa na tmu yake
Ipo namna Manqoba anafelishwa na tmu yake
4m ago
READ MORE β†’
Manqoba alia na matumizi ya nafasi
Manqoba alia na matumizi ya nafasi
38m ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 18 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 18 2026
4h ago
READ MORE β†’
Goals; CFFA 0-4 Yanga (FT)
Goals; CFFA 0-4 Yanga (FT)
16h ago
READ MORE β†’
FT : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL R1
FT : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL R1
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : CFFA vs Yanga, CAFCL R1
Kikosi : CFFA vs Yanga, CAFCL R1
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
Matchday; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 17 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 17 2026
1d ago
READ MORE β†’
Diarra hatihati kuikoa CFFA
Diarra hatihati kuikoa CFFA
1d ago
READ MORE β†’