Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameushauri uongozi wa Yanga kumaliza changamoto zinazoikabili timu hiyo ili kurejeshea makali yake.
Katika mahojiano yake aliyofanya na mtandao wa ShaffihDauda, Zitto ambaye anafahamika ni shabiki wa Simba, amesema soka la Tanzania haliwezi kukua bila ya Yanga imara.
"Yanga walikuwa na tatizo la uongozi, tunafahamu aliyekuwa mwenyekiti wao alipata matatizo kwa hiyo wametetereka kidogo kutokana na hayo," alisema Zitto
"Kinachotakiwa ni wanachama, mashabiki na wapenzi wa Yanga kutafakari namna ya kutoka kwa sababu ukiwa na Yanga legelege huwezi kupata mpira mzuri hapa nyumbani, raha ya mpira ni ushindani na sisi Simba tunataka kushindana na timu bora ambayo imeimarika."
"Mimi nawaombea heri wenzetu wa Yanga, ni jambo la kukaa chini kutafakari na kuweza kuona ni namna gani wanatatua changamoto zilizowakuta.
"Kama ni Manji kurudi au watafute mtu mwingine au watu wengine wa kusaidia klabu yao iende vizuri sio lazima awe mtu mmoja."
Zitto ametoa maoni yake wakati Yanga ikiwa tayari imeanza kuchukua hatua ya kuirejeshea timu hiyo makali yake.
Kupitia Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika Juni 10 2018 ukumbi wa Bwalo la Polisi, Osterbay jijini Dar es salaam, kwa mamlaka waliyopewa na Katiba ya Yanga, wanachama wa klabu hiyo waliipinga barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wao Yusuph Manji.
Tayari Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amemuandikia barua Manji kumjulisha uamuzi huo wa Wanachama ambao wamemuomba arejee kwenye nafasi yake.
Yanga pia iliunda Kamati Maalum ya Mpito kushughulikia changamoto zake za kiuchumi ili kuweza kuhuisha mikataba ya wachezaji pamoja na kusajili wachezaji wapya.
Yanga pia inatarajia kuanza kutumia mfumo mpya wa uendeshaji baada ya Kamati Maalum ya 'mabadiliko' kumaliza kazi yake.

ADVERTISE HERE