Tumejiandaa kushinda dhidi ya TRA United - Masalanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Tumejiandaa kushinda dhidi ya TRA United - Masalanga

Mlinda wa lango wa Yanga Hussein Masalanga amesema wamejiandaa vyema kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya TRA United utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari mapema leo, Masalanga amesema wanatambua ubora wa wapinzani wao wakitarajia mchezo wenye ushindani mkali.

Amesema kwa sasa mipango yao wameielekeza katika kushinda mchezo huo ili kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

"Kwa upande wetu sisi wachezaji, tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huu. Tunaamini kwamba kupitia maelekezo tuliyopewa na mwalimu tutaweza kufanya vizuri na kupata matokeo mazuri”

“Tunacheza dhidi ya timu ngumu yenye wachezaji wazuri, lakini hata sisi tuna wachezaji wenye uwezo na tumejiandaa vizuri kwa mchezo huu."

"Kuhusu ugumu wa uwanja, kwetu sisi kila uwanja tunaochezea una changamoto zake. Hata hivyo, tumejiandaa kukabiliana na changamoto hizo ili kuhakikisha tunafanya vizuri."

"Kuhusu michezo iliyopita, hatutaki kutumia muda mwingi kuangalia yaliyopita kwa sababu tayari yameshapita. Tunachokipa kipaumbele ni mchezo unaofuata, kwani tukijikita sana katika yaliyopita, tunaweza kushindwa kufikia malengo tuliyojiwekea,” alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Manqoba atuma ujumbe kwa wachezaji Yanga 'lazima tupambane kushinda'
Manqoba atuma ujumbe kwa wachezaji Yanga 'lazima tupambane kushinda'
2h ago
READ MORE β†’
Manqoba akiri TRA United wagumu, aweka mkakati wa kuwadhibiti
Manqoba akiri TRA United wagumu, aweka mkakati wa kuwadhibiti
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yapania alama tatu Arusha
Yanga yapania alama tatu Arusha
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
8h ago
READ MORE β†’
Manqoba tunamuamini - Kamwe
Manqoba tunamuamini - Kamwe
22h ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni TRA United
Kituo kinachofuata ni TRA United
1d ago
READ MORE β†’
Karibu tena dimbani Job
Karibu tena dimbani Job
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
Highlights; Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
FT : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’