Mechi za kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) zilihitimishwa jana timu zote 16 zilizofuzu hatua hiyo zikifahamika.
Ni rasmi sasa Yanga inatarajiwa kuwekwa kwenye chungu cha pili katika droo hiyo itakayofanyika Jumatano, Oktoba 28 Cairo, Misri.
Katika chungu cha pili (Pot 2) Yanga itakuwa pamoja na watani zao Simba, Al Hilal na Orlando Pirates. Timu hizi hazitakutana kwenye hatua ya makundi.
Katika droo hiyo zitapangwa dhidi ya timu kutoka chungu cha !, III na IV.
Chungu cha kwanza kina Esperance, RS Berkane, Zamalek na Pyramids.
Orodha kamili ya timu zilizofuzu na vyungu vyao kuelekea droo ya Jumatano ni kama ifuatavyo:
- Chungu cha 1: Esperance de Tunis (Tunisia), RS Berkane (Morocco), Zamalek SC (Misri), Pyramids FC (Misri).
- Chungu cha 2: Simba SC (Tanzania), Yanga (Tanzania), Petro de Luanda (Angola), Orlando Pirates (Afrika Kusini).
- Chungu cha 3: Horoya AC (Guinea), FC Nouadhibou (Mauritania), Club Africain (Tunisia), MC Alger (Algeria).
- Chungu cha 4: Wiliete SC (Angola), Al-Hilal Omdurman (Sudan), Maghreb Fès (Morocco), Colombe Sportive (Cameroon).
Mechi za hatua ya makundi zinatarajiwa kuanza kupigwa mapema tu, mwezi Novemba.

ADVERTISE HERE