Mashabiki wa Yanga wanasubiri utambulisho wa kocha wao mpya anayetua kurithi mikoba ya Manqoba Mngqithi aliyefutwa kazi wiki iliyopita.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga ni kuwa makubaliano yamefikiwa kumrejesha kocha wao wa zamani Sead Ramovic.
Inaelezwa kocha huyo huenda akawasili nchini leo kwa ajili ya kusaini mkataba ili kuanza majukumu yake ya kuwatumikia Wananchi kwa awamu ya pili.
Ramovic ni kocha ambaye tayari mashabiki wa Yanga wanamfahamu baada ya kazi nzuri aliyoifanya kwa muda mfupi kabla ya kutimkia CR Belouizdad.
Baada ya Manqoba kufutwa kazi, mashabiki wa Yanga wengi walivamia kurasa za mitandao ya kijamii za Kocha Ramovic na kocha wa viungo Adnan Behlulovic huku wakituma maoni kwa wingi kwa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said wakiomba warudishwe makocha hao kama upo uwezekano.
Habari njema ni kuwa huenda jambo hilo linakwenda kutimia..!