Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga

Droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) msimu wa 2026/2027 imezua taharuki na msisimko mkubwa miongoni mwa wapenzi wa soka nchini Tunisia na Tanzania, kufuatia miamba ya soka, Yanga SC na Club Africain ya Tunisia, kupangwa Kundi B.

Kundi hilo ambalo tayari wachambuzi wa soka wamelibatiza jina la "Kundi la Kifo," linajumuisha pia miamba mingine miwili ya soka kutoka Kaskazini mwa Afrika: Zamalek SC ya Misri na MC Alger ya Algeria.

Picha na video mitandaoni zinazowaonyesha mashabiki wa Club Africain wakipokea matokeo ya droo hiyo kwa mshtuko hasa baada ya Yanga kutajwa kuwa kundi hilo.

Ingawa timu yao inasifika kwa nidhamu kubwa ya ulinzi msimu huu hali iliyowawezesha kuitoa miamba ya TP Mazembe kwenye hatua ya mchujo lakini wanajua ugumu wa kukutana na Yanga kwenye hatua ya makundi.

Kuongezeka kwa heshima ya Yanga barani Afrika ni miongoni mwa sababu kubwa ya hofu hiyo. Katika misimu minne iliyopita, Yanga imeonyesha ukomavu mkubwa katika mashindano ya CAF.

Mashabiki wa timu hiyo hawajasahau machungu ya kutolewa na Yanga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho 2022/23 katika uwanja wao wa nyumbani wakifungwa bao 1-0 na Wananchi wakafuzu hatua ya makundi katika msimu ambao walikwenda hadi fainali na kukosa ubingwa kwa mujibu wa kanuni baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya USM Alger.

Kwa mujibu wa ratiba ya CAF, miamba hii itakutana mara mbili katika hatua hii ya makundi. Club Africain watakuwa wenyeji wa Yanga SC nchini Tunisia kati ya Desemba 4 na 6, 2026.

Yanga SC watakaribisha Club Africain kwenye mchezo wa pili kati ya Januari 22 na 24, 2027, mchezo ambao utahitimisha hatua ya makundi na pengine unaweza kuamua timu itakayosonga mbele robo fainali.

Kuelekea hatua hiyo ya makundi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba hawaihofii timu yoyote kwenye kundi hilo na wamejipanga 'kubonda na kunyonga' kila atakayepita mbele yao.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’