Gadiel Michael kujiunga na Yanga Disemba

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
4 Aug 2017
Gadiel Michael kujiunga na Yanga Disemba
Uongozi wa klabu ya Yanga, umeachana na mpango wa kumsajili sasa mlinzi wa kushoto wa Azam FC Gadiel Michael na kwa maana hiyo atajiunga na Yanga mkataba wake utakapomalizika mwezi Disemba.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es salaam leo, Katibu Mkuu Charles Mkwasa amekiri ni kweli Gadiel amesaini mkataba wa awali kuitumikia Yanga.

Lakini hivi karibuni kumekuwa na mkanganyiko juu ya mkataba wa mchezaji huyo na klabu ya Azam ambapo Azam imedai mkataba wake unamalizika mwezi Disemba.

Mkwasa amesema Yanga ilifanya mazungumzo na Azam juu ya kutaka kuvunja mkataba wa mchezaji huyo, miezi michache iliyobaki.

Azam imejibu maombi ya Yanga kupitia barua iliyoandikwa na uongozi wa klabu hiyo siku mbili zilizopita.

Hata hivyo Yanga imeachana na mpango wa kumsajili sasa na hivyo atajiunga na Yanga mwezi Disemba akiwa mchezaji huru.

Mkwasa amesema Azam imetaka ilipwe kiasi kikubwa cha pesa kumuachia mlinzi huyo mahiri licha ya mchezaji huyo kubakisha miezi minne pekee.

Kwa maana hiyo ni kwamba Gadiel atajiunga Yanga BURE. Azam FC hawatapata hata senti tano ifikapo mwezi wa 12.

Aidha Mkwasa ameshangazwa na klabu ya Azam kuweka ugumu pale wachezaji wake wanapotaka kujiunga na Yanga tofauti na ilivyo kwa Simba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’