Kikosi cha Yanga kitarejea tena dimbani siku ya Jumapili kuikabili Kagera Sugar katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC.
Mchezo huo wa raundi ya 10 unatarajiwa kupigwa uwanja wa KMC Complex saa 1 usiku.
Baada ya ushindi dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo uliopita, hii itakuwa nafasi kwa Yanga kuendeleza wimbi la ushindi baada ya kupita kipindi kigumu cha kukosa ushindi kwenye mechi mbili.
Aidha kwenye mchezo huo huenda Yanga ikawa tayari ina kocha mpya na pengine atakuwa jukwaani kuwashuhudia vijana wake.
Inaelezwa Yanga imekamilisha mazungumzo na kocha Sead Ramovic ambaye kwa mujibu wa taarifa huenda akatua nchini leo kukamilisha taratibu za kusaini mkataba tayari kuanza majukumu yake kwa awamu ya pili.
Kuna uwezekano mkubwa kocha huyo mpya akaendelea na baadhi ya wataalam waliopo kwenye benchi la ufundi akiwemo kocha msaidizi Simo Dladla ambaye anarajiwa kuiongoza Yanga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar.