Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3h ago
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa

Wachezaji tisa wa Yanga wameitwa tmu za Taifa kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2027.

Ligi Kuu imesimama kwa takribani wiki tatu kupisha kalenda ya FIFA ambapo wachezaji hao wanakwenda kutekeleza majukumu.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha nyota hao kupokea wito kutoka kwa Mataifa yao

Nyota wa Yanga walioitwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ni Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Clement Mzize na Seleman Mwalimu.

Nyota wa kigeni wanaokwenda kwenye majukumu ya timu za Taifa ni Djigui Diarra (Mali), Peter Shalulile (Namibia), Albert Kangwanda (Zambia) na Hussein Zakuane (Comoro).

Wakati wachezaji hao wakikosekana, Kamwe amesema kocha mpya wa timu hiyo ataandaa program maalum ya mazoezi kwa ajili ya wachezaji waliobaki ili kujiandaa na mechi zinazofuata baada ya mapumziko ya FIFA.

Kamwe amesema uongozi utafanya tathmini mapendekezo ya kocha kuona kama wanaweza kuweka kambi maalum nje ya nchi ili kumpa nafasi kocha mpya kuweka sawa mikakati ya maboresho ya timu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
6m ago
READ MORE β†’
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
4h ago
READ MORE β†’
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
17h ago
READ MORE β†’
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
1d ago
READ MORE β†’
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Kocha tayari amewasili tutamtambulisha wakati wowote - Kamwe
Kocha tayari amewasili tutamtambulisha wakati wowote - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 02 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 02 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NBC PL (FT)
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NC PL, Nov 1
FT : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NC PL, Nov 1
1d ago
READ MORE β†’