Msimu uliopita Yanga ilicheza mechi zake za nyumbani hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) kwenye uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar. Taarifa za ndani ni kuwa Yanga imepanga kutumia tena uwanja huo msimu huu.
Baada ya uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa, ni uwanja wa Uhuru pekee ambao unakidhi vigezo vya CAF kutumika kuanzia hatua ya makundi.
Dimba la Azam Complex ambalo Yanga wamelitumia kwenye hatua za awali, halijakidhi vigezo.
Hata hivyo baada ya watani zao Simba kuchagua uwanja wa Uhuru kama uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi za ligi na hata ligi ya mabingwa, ni wazi mafahari hawa hawatatumia uwanja mmoja.
Aidha uwepo wa timu nne za Tanzania ambazo zimefuzu hatua ya makundi CAFCL na CAFCC ni wazi italazimu timu nyingine kuchagua viwanja tofauti ili kupunguza mzigo dimba la Uhuru.
Uwanja wa New Amaan Complex sasa uko tayari kutumika tena baada ya ukarabati kukamilika.