Tarehe kama ya leo, miaka mitatu iliyopita, mashabiki wa Yanga walishuhudia timu yao ikiandikisha historia pale uwanja wa Benjamin Mkapa.
Uwanja wa Mkapa uligeuka kuwa sehemu ya burudani ya upande mmoja baada ya Yanga SC kuichapa Simba SC mabao 5-1 katika mchezo ulioacha gumzo kubwa kwenye ulimwengu wa soka la Tanzania.
Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yaliwekwa kambani na Kennedy Musonda, Maxi Nzengeli aliyefunga mawili, Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua aliyeweka kambani bao la tano kupitia mkwaju wa penati.
Maxi, Aziz Ki na Pacome bado ni sehemu ya kikosi cha Yanga huku Kennedy Musonda akirejea kwao Zambia.
Ni Novemba 05, kumbukumbu hii itaendelea kuishi kwa miaka mingi pengine mpaka pale itakapoandikwa nyingine...!
ADVERTISE HERE