Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa beki na nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto.
Misimu sita Mwamnyeto yuko kwenye familia ya Wananchi. Kwa sasa ndiye mchezaji mwandamizi zaidi aliyebaki kikosini.
Amebeba zaidi ya mataji 15 akiwa nahodha wa mabingwa hao wa kihistoria.
Pamoja na ukosoaji anaokumbana nao mara kwa mara, lakini ameendelea kuwa imara na kutekeleza majukumu yake kama kiongoni wa wachezaji.
Sio kwa bahati mbaya kwake kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa miaka sita.
Tunamtakia kila kheri katika siku hii ya kumbukumbu muhimu kwake.
HAPPY BIRTHDAY MWAMNYETO...!
ADVERTISE HERE