Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki mashabiki wa timu yake wanaamini bado hajafikia asilimia 100 ya ubora ambao alionyesha misimu miwili iliyopita kabla ya kusajiliwa na Wydad CA.
Hata hivyo licha ya ukweli huo, ni kwamba Aziz Ki ameanza vyema majukumu yake kwenye kikosi cha Wananchi kutokana na mchango wake kwa mujibu wa takwimu.
Katika mechi nne za ligi alizocheza, Aziz Ki ametoa asisti katika mechi tatu akiwa na asisti tatu nyuma ya Hussein Zakouane ambaye ndiye kinara wa asisti kwenye kikosi cha Yanga akiwa nazo nne.
Mchezo pekee ambao Aziz Ki hakuhusika kutoa asisti ni dhidi ya Kagera Sugar ambao alitolewa kwa kadi nyekundu dakika 18.
Wakati huu ambao ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA, Aziz Ki atakuwa na muda wa kujiimarisha zaidi kuelekea kwenye ratiba muhimu ya mechi za ligi ya mabingwa hatua ya makundi.