Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar kuweka kambi ya muda mfupi kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA.
Maandalizi hayo ni maalum kwa ajili ya mechi za ligi zitakazoendelea baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA na zaidi ni kujiandaa na hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Fadlu kuanza kazi Zanzbar
Taarifa zaidi zimebainisha kuwa Kocha Mpya wa Yanga Fadlu Davids ataanza rasmi majukumu yake visiwani Zanzibar baada ya kutambulishwa.
Fadlu anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ndani kabla ya utambulisho.
Inaelezwa tayari Yanga imefikia rasmi makubaliano nae kurithi mikoba iliyoachwa na Manqoba Mngqithi.
Mchezo utakaofuata baada ya mapumziko ya FIFA Novemba 20 ni dhidi ya Polisi Tanzania ukitarajiwa kupigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.