Tulieni, tutakuwa na kikosi imara msimu ujao - Nyika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jun 2018
Tulieni, tutakuwa na kikosi imara msimu ujao - Nyika
Wakati suala la usajili likifanywa kimya kimya, uongozi wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki wao kuvuta subira huku ukiwahakikishia watakuwa na kikosi imara msimu ujao.

Yanga kwa sasa ipo bize ikisaka wachezaji wa kuimarisha timu hiyo tayari kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika, amesema kamati yake kwa kushirkiana na kamati maalum iliyoundwa inaendelea na mambo yao na watakuwa na kikosi imara msimu ujao.

"Mashabiki wanatuamini na waendelee kutuamini, hatupo kimya tunaendelea na mambo yetu ya usajili, tutakuwa na kikosi imara msimu ujao ambacho kitaweza kurudisha makali na ubingwa wetu pia," alisema Nyika.

Alisema usajili wanaofanya unatokana na mapendekezo ya benchi la ufundi na hawasajili kwa sifa au kufuata mkumbo.

"Tunasajili wachezaji kulingana na matakwa ya kikosi chetu, hatusajili kwa kufuata maneno ya watu au ushabiki, tunataka wachezaji wenye uwezo na ambao wataisaidia timu," amesema Nyika.

Nyika amesema kamati yao ipo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji kwa ajili ya kuwasajili, lakini mambo yao wanayaendesha kimya kimya.

"Wapo wachezaji ambao tumefikia nao kwenye hatua nzuri, tunataka tukikamilisha kila kitu ndipo tuwatangaze, mashabiki na wanachama wa klabu yetu wasiwe na hofu kila kitu kinaenda sawa," aliongeza Nyika.

Yanga tayari imeanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wake wa hatua ya makundi dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo utachezwa Julai 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’